Team LUPUSTZ, kwa umoja wao na ushirikiano wao LUPUSTZ ORGANISATION na LUPUS AWARENESS AND SUPPORT FOUNDATION (LASF) Walibarikiwa kupata mwaliko wa Mkutano wa NACONGO ndani ya siku mbili mfululizo jijini dodoma.
Mnamo tarehe 29 - 30 September 2021
Kwa hakika tulioweza kuhudhuria Mkutano huu Kama LUPUSTZ ORGANISATION tumeweza kujifunza mengi mno kwanzia namna ya kuendesha organisation, kusimamia mapato ya organisation, uongozi, Kodi za mwaka, kutuma report ya kila mwaka ili wajue Kama org ipo active nakadhalika.. hata kama hampati misaada tunatumia hela zetu kwenye kufanya awareness na mikutano yetu wenyewe.
Pia networking na other organisations.. uncle @Baba Debra Mr. Leslie ambaye ndio Katibu Mkuu wa LUPUSTZ aliweza kuwasilisha mapendekezo yetu mbele ya muhadhara na soon tutaingia katka utekelezaji juu ya kuondolewa Kodi Kwan organisation za Lupus Ni charitable so ni ngumu kulipa Kodi sio Kama wanaofanya biashara!!
Mkutano huu 29 September mgeni rasmi alikuwa Dr. Dorothy Gwajima minister of Health na tarehe 30 September 2021 mgeni rasmi alikuwa President Samia Suluhu... Pia huu Mkutano uliandaliwa na serikali so kamati ya maandaliz uliweza kutambua kuwa LUPUS ni Kati ya ulemavu usioonekana na kukawa na nafasi yetu maalum kwa wagonjwa wa LUPUS hiyo ni bonge la hatua kwetu Sisi tunaopigania Haki za watu wanaoishi na ugonjwa wa Lupus nchini TZ...Kwa upande mwengine Hajrrath Mohammed ambaye ni LUPUSTZ Organisation Active Member & Advocate alipata kutumia fursa kwa kutoa awareness ya Lupus 🙌🏾💜